Ndege ya Kenya Airways yapata misukosuko Dar........Soma zaidi hapa

Ndege ya Kenya Airways safari namba KQ-482, iliyokuwa ikitua katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam iliacha njia (runway) kabla ngazi za dharura kufunguka na waliokuwa ndani kulazimika kutoka kwa dharura.

Waliokuwepo eneo la tukio wanasema injini moja ya ndege hiyo aina ya Embraer E190,iliyokuwa safarini kutoka Nairobi kwenda Dar Es Salaam, ilipata hitilafu (engine failure) na kukosa nguvu (thrust) ya kusimama katika hali ya kawaida huku mvua kubwa ikinyesha. Ingawa uchunguzi utatoa jibu kamili. 

Mmoja wa abiria wa KQ482 akisaidiwa kutoka katika ndege huyo huku ngazi za dharura  zikiwa zimefunguka. Picha na Miguel Martinez.

Akizungumza nasi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi, amethibitisha kutokea kwa mkasa huo na kueleza kuwa halikuwa tatizo kubwa na kwamba abiria na wafanyakazi wa ndege hiyo wako salama.

Hata hivyo walioshuhudia na baadhi ya abiria waliokuwemo katika chombo hicho wamenukuliwa wakisema walipata mshtuko na wengine majeraha madogo.

Ndege kadhaa za safari za ndani na pia kimataifa ziliagizwa kutua Zanzibar wakati tukio likishughulikiwa, kabla ya ndege kuvutwa na kuwekwa sehemu salama na uwanja kufunguliwa upya.

Embraer ni ndege inayotengenezwa Brazil, na wataalam wanasema aina hiyo ya dharura si jambo la ajabu.
Powered by Blogger.