Watu 2 Wanashikiliwa na Polisi kwa Kukutwa na Meno ya Tembo Simiyu

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo sita ikiwa ni pamoja na silaha moja, huku mtu mmoja akishikiliwa kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa chekechea mwenye umri wa miaka saba.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishina Msadizi Mwandamizi Onesmo Lyanga amesema Oktoba 10 mwaka huu majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Bumela kata ya Bumela wilayani Itilima askari polisi wakishirikiana na askari wa wanyamapori kutoka Maswa Game Reserve wakiwa katika msako waliwakamata wawindaji haramu.
Waliokamatwa ni Sendama Musa na Busule  Nzugu wakiwa na pembe mbili za ndovu zenye uzito wa kilo 6 ikiwa ni pamoja na silaha moja yenye uwezo kufanya kazi kama silaha aina ya short gun na kisha kumtaja mtuhumiwa aliyekutwa na silaha hiyo kuwa ni Masanja Machungwa mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa  katika kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.

Katika hatua nyingine Kamanda Lyanga ameongeza kuwa mbali na tukio hilo la kukutwa nyala za serikali pamoja na silaha polisi mkoani hapa wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Musa Noni kwa tuhuma ya kumbaka mtoto mwenye umri miaka 7 ambaye anasoma chekechea katika shule ya msingi Ipililo wilayani Maswa.

Aidha Kamanda Lyanga amewataka wamiliki wa magari na mikokoteni mkoani hapa kuhakikisha wanaweka viakisi mwanga katika vyombo vyao pamoja na kudhibiti mwendo kasi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti ajali mkoani humo.
Credit: ITV
Powered by Blogger.