Napenda na kupendwa na wanawake wenzangu kimapenzi

Naomba ushauri: Wengi wanadhani nimependa kuwa hivi au tunaopenda wenzetu wa jinsia moja tumetaka.La hasha!!!Mimi ni mrembo sana,kuanzia sura, umbo, nina akili lakini pia nimekuzwa familia ya dini sana. Nikiwa sekondari form 2 nilitokea kumpenda sana dada mmoja yeye alikuwa Advance. Alinipenda sana pia ,ila kuliishia kukumbatiana tu.

Nikiwa Advance nilipendwa na binti mmoja,niliogopa sana maana alikuwa ananipa care kupita kiasi.Uhusiano ulifika mbali zaidi mpaka nikawa mtumwa wa mapenzi.Sikuweza kula wala kufanya chochote bila yeye.Nilikuja kugundua alianza uhusiano mpya hivyo tukaachana soon nilipomaliza A level.

Nikiwa chuo nilipata boyfriend kwa mara ya kwanza.Nilijaribu sana kuwa nae karibu maana alinipenda sana na alinipa kila kitu.Sikuwa najisikia mapenzi hata kidogo.Wengi waliniona nina bahati maana alikuwa mzuri sana, mchapa kazi na ana akili zaidi ila tu hajatulia.

Nililigundua hilo nikiwa ndani ya uhusiano. Japo kila nikimkamata anasema wanawake ndio wanamtaka ila hana time nao. Pamoja na yote kwa kweli alinipenda. Maombi yangu kwa Mungu yalikuwa na mm niweze kuwa in like na mwanaume. Niliomba sana na kufunga.Nilijitenga na wanawake. Nilipomaliza chuo niligundua jamaa alikuwa bado hajatulia tukaachana japo mwenyewe mapenzi hayakuwa kihivyo. Mara nyingi nilikuwa namkumbuka my x,nilikuwa mnyonge sana.

Nilijihisi kwa huyo bf mimi nilikuwa kama sex mashine. Nilikuwa mwaminifu sana ndani ya mahusiano.Baadae tukaachana, mm nikaamua kumdate mke wa mtu.Alinipenda mwenyewe. Sikuwahi kumwambia chochote juu yangu.Ila kila wakati aliniita mpenzi,honey darlin na kunikiss kila mara.Tulifall in like. Ila nilijilaumu kwa kuwa sikutamani niwe na mwanamke tena ila sasa uhusiano na wanaume ulikuwa mgumu ,napendwa ila kupenda hakukuwepo. Nikaona nitavunja ndoa ya watu nikawa namkimbia. Nikajikuta nafall tena kwa mke wa mtu ambae alikuwa rafiki yangu.

Kila wakati aliniletea zawadi na kuniambia ananifeel sana. Tulidate kwa muda kidogo nikaanza kumkwepa maana alianza kumchukia mumewe.Akiamka break ya kwanza kwangu. Ananipeleka hoteli za kifahari .Ila pia alikuwa kanizidi sana umri. Nilipata shida sana kujitoa kwenye penzi lake maana aliapa kuniua nikimuacha. Alinipenda kiasi cha kujitoa ufaham.Nilifanikiwa kumkwepa karibia miezi 8 hv.Namba ya simu nikabadili.Tangu wakati huo naendelea kupata shida maana nimekuwa heart surf.

Nikiumizwa tu na boyfriend kidogo huwa sirudi tena. Nasali sana hii hali iniondoke lakini wapi. Naumia sana, Sijui nifanyeje.

Najua ni kinyume cha jamii na pia dini.Ila mimi sipendi pia hali hii. Mimi sio tom boy na hata mtu akiniona hawezi kudhani.Nimejikuta napendwa na wanawake wengi ,sijui kwa nini pia,huwa sijawahi kumtongoza mwanamke yeyote ila wao hunianza. Ninapokuwa na mwanamke kwenye mahusiano nasikia raha na moyo unarelax.Nifanyeje???
Powered by Blogger.