Mwalimu ahukumiwa kwa kumpa mwanafunzi wake wa Madrasa Mimba...

Mwalimu wa chuo cha madrasa kilichopo Chakechake Pemba Said Khamis ameanza kutumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 15 jina linahifadhiwa.
Mwendesha Mashtaka wa Mapinduzi ya Zanzibar Ali Bilal aliiambia Mahakama mbele ya hakimu kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo miezi mitatu iliyopita.

Alisema baada ya ucgunguzi wa DNA uliofanywa Tanzania bara ulionyesha kuwa  asilimua 96 mtuhumiwa ndiye aliyempa ujauzito mwanafunzi huyo.

Alisema mtuhumiwa atatumia chuo cha mafunzo jela  kwa miaka saba na atakapotoka atalazimika kulipa fidia ya milioni moja ikiwa ni fundisho kwa wengine kuacha ufanya vitendo kama hivyo kwa wanafunzi wa vyuo na madrasa.
Powered by Blogger.