Diamond aanika ukweli 'Wema, Jokate na Penny hawakuwatayari kuzaa na mimi'

Akizungumza kwenye kipindi cha Live Chumba cha Habari kinachorushwa na Global TV online, Msanii wa muziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alieleza jinsi wapenzi wake wazamani ambao ni Mwigizaji Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na matangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Diamond alifunguka baada ya kuulizwa kwamba amekuwa akitangaza kupenda watoto lakini kwa nini hana hata wa dawa licha ya kuwa na uhusiano  na wanawake tofouti..tofauti.

Diamond: “Ni kweli napenda watoto lakini siwezi kupata mtoto peke yangu bila mwenzangu. Lazima kuwe na mwenzangu ambaye tutakubaliana.“Nilichojifunza ni kwamba wenzangu hawakuwa tayari katika hilo hivyo wakawa wanachengachenga.”

Diamond aliendelea kueleza kuwa mwanadada Penny aliwahi kupata ujauzito wake mara mbili.

 “Ukweli Penny ningezaa naye, aliwahi kuniambia ana mimba yangu, sikuamini, nikampeleka hospitali kupima ikawa kweli. Kesho yake niikamnunulia gari, nikamwambia mama tulia. Siku mbili tatu akasema mimba imetoka.

“Nikaja nikamjaza kingine cha pili (mimba), nayo baada ya muda akaja kuniambia imetoka. Nikaona huyu mzinguaji, nikammwaga. Lakini iliniuma sana.“Kwa wengine (Jokate na Wema) walikuwa wakinichenga tu bila sababu, unamuona huyu hataki kubeba mimba yangu. Mtu kwa mdomo anasema kwamba yuko na wewe kikamilifu lakini kwa matendo unaona siye.

“Lakini kusema ukweli kabisa natamani sana kuwa na mtoto.
“Hapo juzikati nilitaka kuoa, kila kitu kilikuwa sawa, nikaja kubadili mawazo.”
Swali: ”Ulitaka kumuoa nani?”Diamond: “Ah! Siwezi kumsema hapa. Diamond alimaliza.
Powered by Blogger.