Liverpool yakubali kichapo cha bao 2 kutoka kwa Chelsea ........

CHELSEA imeifunga Liverpool mabao 2-0 Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na kufufua matumaini ya ubingwa.

Mabao ya Chelsea inayofundishwa na Mreno Jose Mourinho yamefungwa na Demba Ba dakika ya 45 na ushei Willian aliyemalizia kazi nzuri ya Fernando Torres dakika ya 90 na ushei.


Chelsea sasa inatimiza pointi 78 baada ya kucheza mechi 36 sawa na Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 80, wakati Manchester City yenye pointi 74 za mechiu 34 ni ya tatu.

Mchezaji wa liverpool Steven Gerrard akijaribu kuchukua mpira kwa kocha wa Chelsea manager Jose Mourinho.
Dem ba BA akiifungia Chelsea goli la kwanza


Maandalizi ya mashabiki wa Liverpool wakiwa wanaamini ushindi ni wao kabla ya mechi kuanza.

Mashabiki wa Liverpool wakipiga picha katika sanamu ya David Moyes

Powered by Blogger.