Mwanamke huyu agundua dawa ya kuzuia mume wake asichepuke

Msichana aliyetajwa kwa jina la Abbie Bartlett, wa Ibiza Hispania, amewashangaza wengi baada ya kumvalisha mpenzi wake Leon Connolly fulana maalum yenye ujumbe unaowaponda wasichana wengine na kumsifia yeye kwa lengo la kujihami na wezi wa penzi lao.Abbie alifanya hivyo baada ya kuona kuwa mpenzi wake anataka kusafiri na kwamba wangekuwa mbali kwa muda mrefu hivyo alitaka maandishi pekee yawe ujumbe wa kutosha.
Nampenda mpenzi wangu Abbie, nawachukia wasichana wa Ibiza, kwa hiyo tafadhali kaa mbali na mimi.

Yanaeleza maandishi yaliyo kwenye fulana hiyo ikiwa na picha
Picha ya mpenzi wake akiwa amevaa fulana hiyo ilisambaa haraka kwenye mitandao ya kijamii hali iliyomfanya msichana huyo kuogopa akiamini kuna wasichana wangetaka kumchallenge kwa kumchukua makusudi mpenzi wake.

Nilipoenda kuchapisha fulana hiyo na kuelezea nilichotaka naapa waliona nilikuwa mwehu. Msichana huyo aliimbia North News.

Kwa upande wa Leon yeye alidhani mpenzi wake anatania lakini baadae aligundua yuko serious na anakiri baada ya kuvaa anaona ni poa tu.

Mwanzo nilijiuliza yuko serious?
Alitaka niivae nikienda kwenye club zote kubwa kama Pacha n.k. Lakini sasa hivi ninaichukulia kama utani na nimefurahishwa vya kutosha kuendana nayo. Hivyo ndivyo uhusiano wetu unavyokwenda… Watu wanasema kuvaa fulana hiyo inaweza kuwavutia zaidi wasichana kufanya challenge. Nimekuwa nikicheka kuhusu hilo, Abbie ni msichana pekee kwangu na wote tunalifahamu hilo.

Powered by Blogger.