Isabela amchana mama Wema kwa kuingilia mapenzi ya mwanae..

MSANII wa Filamu na Muziki Bongo, Isabela Mpanda amemvaa mama wa msanii mwenzake, Wema Sepetu, Miriam Sepetu na kumtaka aache kuingilia mapenzi ya mwanaye kwani mapenzi hayaingiliwi.
Msanii wa Filamu na Muziki Bongo, Isabela Mpanda.

Akistorisha na gazeti hili, Isabela alisema siku zote unaopenda ni moyo siyo mwili kwa hiyo mama Wema kama anataka mwanaye aachane kabisa na Diamond basi amtoe moyo uliompa nafasi mwanaume huyo.
Mama mzazi wa msanii maarufu bongo, Wema Sepetu.

“Mama Wema kama mzazi anatakiwa akae kimya, amuache mwanaye moyo wake ufanye utakavyo maana kutoa maneno na kufanya sherehe kwa sababu ya mwanaye ameachana na Diamond siyo sawa, akumbuke kwamba Diamond naye ana wazazi, hivi mama yake anajisikiaje jamani?” alihoji Isabela.



Powered by Blogger.