Maazimio 8 ya UKAWA Kukabiliana na Prof. Lipumba na Msajili wa Vyama
Umoja wa Katiba ya Wananchi umedhamiria kwenda mahakamani kumshtaki Prof. Lipumba na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF).
Katika kikao walichofanya jana, UKAWA walipitisha maazimio kukabiliana na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF. Maazimio hayo ni pamoja na;-
- Hatumtambui Prof. Lipumba kama mwanachama wa CUF na Mwenyekitimwenza wa UKAWA
- UKAWA wanautambua uongozi wa Julius Mtatiro na Maalim Seif
- Wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
- Wenyeviti wa mitaa, vijiji, Madiwani, Wabunge wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
- Wabunge wote wanaomuunga mkono Prof. Lipumba watatimuliwa ndani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
- Ushirikiano wa kisiasa Tanganyika na Zanzibar utashughulikiwa na UKAWA
- Mawakili wa UKAWA watamfunguliwa mashtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa matumizi mabaya ya madaraka na
- Mawakili wa UKAWA watamfungulia mashtaka Prof. Lipumba.
Kwa upande wake Prof. Lipumba aliwataka wanachama wa CUF kuwa wamoja na kusema kuwa yeye hajali kuhusu UKAWA kikubwa anachoangala ni kuijenga upya CUF.