Mwanafunzi Kidato cha Nne Anusurika Kifo Akijaribu Kutoa Mimba

Mwanafunzi wa kidato cha nne Butinzya sekondari Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita amenusurika kupoteza maisha wakati akijaribu kutoa mimba aliyodai alipewa na mwalimu wake.

Akizungumza akiwa amelazwa katika zahanati ya Msonga iliyopo mjini Ushiromba leo mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17  alimtaja mhusika kuwa ni mwalimu wake aliyeanza mahusiano naye tangu mwaka 2015 na kuwa anampatia zawadi ndogondogo na fedha Sh 10, 000 hadi 15, 000 za kujikimu.

“Nilibeba ujauzito mwezi Juni mwaka huu, nilipomweleze ndipo akaamua kunipeleka hospitalini hapo kutolewa, lakini ilipofika saa 3:00 usiku tumbo lilianza kuniuma huku damu zikinitoka kwa wingi niliamua kumweleza rafiki yangu ninayekaa naye akaaite walimu waje kunisaidia ndipo waliponileta hospitalini hapa,”alisema Kiura
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Msonga kitengo cha wazazi  wazazi, Dk Makopudo Hergard alisema mwanafunzi huyo alipokelewa majira ya saa 7:30 usiku akiwa na hali mbaya huku akitokwa na damu nyingi baada ya kutoa mimba.

Dk Hergard alisema baada ya kumuhoji tuligudua mwanafunzi huyo alitoa mimba lakini mimba haikutoka yote hivyo walimwekea dripu tano za maji na kumchoma sidano ya kukata damu hali na hivi sasa hali yake inaendelea vizuri lakini amepewa rufaa kwenda hospitali ya Wilaya kwa ajili ya uchuguzi zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema taarifa za mwanafunzi huyo kunusurika kifo anazo na kwamba taratibu zilizopo ni kumtafuta mwalimu anayehusishwa na kitendo hicho na atakapokamatwa hatua za kisheria dhidi yake zitafuata.
Powered by Blogger.