Donald Trump Atangaza Sera Zake Kuhusu Uhamiaji

Mgombea kiti cha Urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump ametangaza sera zake kuhusu uhamiaji wakati wa hotuba yake huko Phoenix, Arizona.

Trump aliwataja watu kadhaa ambao anasema waliuawa na wahamiaji haramu na kusema kuwa nchi yake ina haki ya kuchagua ni raia gani wa kigeni wanaruhusiwa kuingia.

Pia aliahidi uhusiano mpya na taifa la Mexico.
Trump ameyasema hayo saa kadha baada ya ziara yake nchini Mexico kwa mazungumzo na Rais Enrique Pena Nieto.

Aidha amesifu mchango unaotolewa na Wa Marekani wenye asili ya Mexico, lakini akatetea mpango wake wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili.
Powered by Blogger.