Wafanyakazi wa TMA watakiwa kutumia mfumo wa kisasa kuhifadhi taarifa muhimu za ofisi
Watumishi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, (TMA) wametakiwa kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika kuhifadhi taarifa zao muhimu na badala yake kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa kieletroniki.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Pof. Makame Mbarawa jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wafanyakazi hao na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kununulia karatasi.
“Katika ofisi zenu nimeona kila mtu anakomputa ni jambo zuri hivyo zitumieni katika kuhifadhi taarifa muhimu za taasisi yenu kwa mfumo wa kieletroniki” alisema Mhe.Prof.Mbarawa.
Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika kujenga mkongo wa taifa wa kuhifadhi taarifa muhimu hususani za serikali pamoja na Taasisi zake hivyo ni budi waanze kuutumia mkongo huo kwa kuhifadhia taarifa zao.
Pia aliongeza kwa kuwataka watumishi kuwa waadilifu,wachapaka kazi ,wabunifu na kuwa na uwazi baina ya watendaji wa juu na watumishi wa ngazi ya chini kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mikoani .
“Watanzania wanamatarajio mengi kutoka kwetu katika kukuza uchumi wa nchi hivyo ni wajibu wetu kutimiza matarajio yao kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo miundo mbinu imara ya barabara, bandari ,shirika la ndege la kisasa na utabiri wa hali ya hewa wenye uhakika ” alisema Mhe.Prof.Mbarawa.
Prof.Mbarawa alitoa wito kwa kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano kila mmmoja kujituma katika eneo lake la kazi ili kuleta matokeo yaliyobora na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kufikia uchumi wa kati.