Mkuu wa shirika la UN amshutum Trump

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Kibinadamu ameshutumu sera za mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, akisema ni sawa na ushenzi.

Zeid Raad al-Hussein, ingawa hakumtaja Bw Trump moja kwa moja, alizungumzia hatua ya mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kuunga mkono mateso pamoja na sera zake kali dhidi ya Waislamu.

“Ushenzi na ulokole si thibitisho la uongozi thabiti,” Hussein alisema.

Kamishna huyo pia amekosoa mpango wa mgombea mwengine Ted Cruz wa kuweka mpango wa kupeleleza maeneo wanamoishi Waislamu.
Powered by Blogger.