Kamati ya kuchunguza mkataba wa Lugumi hadharani

Kamati ya kudumu ya bunge inayoshughulikia hesabu a serikali (PAC) imeunda kamati ndogo ya watu tisa itakayochunguza kwa kina mkataba uliozua utata wa sh 37 billioni uliongiwa baina ya Jeshi la polis na lugumi Enterprises.

Pande hizo mbili, Jeshi la polis na Lugumi Enterprises ziliingia mkataba huo kwa ajili ya kufungua vifaa 108 vya kuhifadhia alama za vidole ktika vituo vya polisi.
Akizungumza na wanahabari leo mjini Dodoma, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Aeshi Hilary amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa siku 30, kuanzia Jumatatu ijayo.

Wajumbe tisa wa kamati hiyo ni Japhet Hasunga (Vwawa-CCM), Wengine wa CCM ni Livingstone Lushinde(Mtera), Stanslaus Mabula(Nyamagana), Haji Mponda(Malinyi) na Hafidh Ali Tahir(Dimani).

Wabunge wa upinzani waliopo katika kamati hiyo ni Nahenjwa Kaboyoka(Sae Mashariki-Chadema), Musa Mbaruk(Tanga Mjini-CUF), Tuza Malapo(Viti Maalum-Chadema_ na Khadija Massor Ali(Viti Maalum-CUF).
Powered by Blogger.