Wema Sepetu azua gumzo mtandao baada ya kumuita Diamond "kaka"

Huku macho na masikio ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yakiwa kwenye bunge la katiba linalojadili lile sakata la tegeta ESCROW, mwanadada Wema sepetu ameamua naye kuzua gumzo kwenye mtandao baada ya kutoa salamu ya pongezi kwa kijana Naseeb al maarufu kama Chibu dangote ama Diamond platnumz kwa ushindi wake wa tuzo 3 kwenye tuzo za Channel O MUSIC AWARDS zilizofanyika huko Afrika ya kusini akitumia neno KAKA katika sentensi yake kitu ambacho kimezua minong’ono ya hapa na pale kwenye mtandao ule maarufu wa kijamii wa picha nchini.

Katika post yake hiyo Wema aliandika

 “…Hongera tele ziende kwa kaka platnumz... I must say he did Tanzania proud..”   na kufanya watu waanze kufunguka ya kwaio ya moyoni kuhusu kauli hiyo na baadhi yao walisema haya.


MELA : “Leo kawa kaka!!!!!! Aiseeee mapenz ya mastaa mafupi kama mkia wa kondoo”


“ LILY: “et kaka plutnums heheheheh wema bwana”


“PIERE: mara hii kaka tena?? Ohhhhhh”


ANNA: “hao ni wakuwaacha kesho.tu.watakua tena pamoja”

Katika tuzo hizo, diamond alisindikiwa na anayesemekana kuwa kipenzi chake cha sasa, mwanadada Zari ktukoa nchini Uganda, pamoja na mama yake mzazi na team ya wasafi.


Nini maoni yako mdau kuhusu ishu hii?
Powered by Blogger.