TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTOTO MDOGO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ANGEL RAMADHANI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA KILICHOPO JIRANI NA NYUMBA YAO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.11.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO IKUTI, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, MTOTO HUYO ALITAMBAA KUELEKEA KWENYE KISIMA HICHO NA NDIPO ALIPOTUMBUKIA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.AIDHA, WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO ALIKUWA JIKONI ANAPIKA NA KUMUACHA MTOTO HUYO AKIWA ANACHEZA NA NDIPO ALITAMBAA NA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA KILIKUWA JIRANI NA NYUMBA YAO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. AIDHA, ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA/VYOO NA KUFUKIA MASHIMO YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MTU MMOJA MKAZI WA KATUMBA WILAYA YA RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALEX PHILIPO (25) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 22 SAWA NA UZITO WA GRAMU 110 KWENYE MFUKO WAKE WA SURUALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 26.11.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KATA YA IBIGI, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Imesainiwa na;
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.