Shabiki afariki dunia katika mechi ya Atletico Madrid na Deportivo La Coruna huko Hispania.

Shabiki mmoja amefariki dunia huko nchini Hispania kufuatia vurugu zilizotokea muda mfupi kabla ya mchezo kati ya Atletico Madrid na Deportivo La Coruna.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alifariki dunia baada ya kupata shinikizo la damu wakati akiwa miongoni mwa wtau waliokuwa katikati ya vurugu zilizotokea kati ya mashabiki wa timu zote mbili.

Awali uongozi wa ligi ya Hispania ulijaribu kuahirisha mchezo huo lakini jaribio la kufanya hivyo lilizuiliwa na Shirikisho la soka la Hispania.

Vurugu kati ya mashabiki zilitokea saa tatu kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki kadhaa waliumia wakiwemo watu 10 ambao walipata majeraha yaliyohitaji kuwahishwa hospitalini.

Viongozi wa juu wa klabu zote 20 za ligi kuu ya Hispania wametoa tamko la kukemea vurugu zilizotokea baina ya mashabiki wa Deportive na Atletico Madrid nab ado haiajfahamika kama kuna hatua zozote zitakazochukuliwa kwa timu hizo kufuatia vurugu zilizotokea.

Mchezo huo uliendelea kama kawaida ambapo Atletico Madrid walishinda 2-0 baada ya mabao yaliyofungwa na Saul Nigez na Arda Turan.
Powered by Blogger.