Mvua zinazoendelea kunyesha zasababisha mafuriko Ifakara na kivuko kwenda mrama...
Mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini zimesababisha mafuriko katika mji wa ifakara mkoani Morogoro na kuharibu miundo mbinu ya barabara,madaraja na kivuko cha ifakara kwenda mrama mkoani humo.
Akizungumza mmoja wa abiria waliokwama kwa siku nne kutokana na kukosa usafiri wa kuelekea Mrimba kutoka mji mdogo wa Mwembetogwa Ifakara,Mei Ibogo anasema sehemu kubwa ya barabara inayoelekea Mrimba imejaa maji na barabara hiyo haipitiki kwa sasa.
Anasema ameshuhudia sehemu kubwa ya barabara kuelekea kivuko cha Mto Kilombero kinachovusha abiria kwenda Malinyi kutoka Ifakara imechukuliwa na maji na hivyo abiria wanaoelekea mrimba na mahenge kukosa usafari kutokana na uharibifu huo.
Mei amesema yeye pamoja na abiria wengine wameshauriwa kusubiri maji ya pungue ama watumie usafari wa mitumbwi japo kwa wale wanaofahamu kuogelea kwakuwa maeneo mitumbwi hiyo inapita kumekuwa na changamoto ya kuzidiwa na maji na kupelekwa katika mwelekeo mwingine.
Naye mkazi wa Mwembetogwa Khamisi Mumbira pamoja na kueleza kuwa mafuriko ya mwaka huu kuwa makubwa kuyashuhudia amesema usafiri ambao waweza kutumika sasa kutoka ifakara kwenda Mrimba ni treni ama trekta japo ameitupia lawama serikali kwa kutoshughurikia miundo mbinu ya barabara katika eneo hilo