Alikiba aliahidi kuachia wimbo mpya soon, je ni ujio wa collabo na Fally?

Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao kila siku hukutana na swali la ‘lini unatoa wimbo mpya’, kutokana na ukimya wa muda mrefu japo jibu lake huwa moja ‘soon’.

Tunda man wa Tip Top Connection ni kati ya marafiki wa karibu wa Alikiba, na leo kupitia Instagram ameweka picha ya Alikiba akiwa na Fally Ipupa na kuandika:
“Bonge la ngomaaaaaaaa dah big up @alikiba4real big up @fallyipupa01 hatari naiskiliza kila mda new hit unarudi kwa vurugu nyingi”, hii inamaanisha kuna ujio wa collabo ya Alikiba na Fally? Kama ndivyo basi naamini itakuwa ni ‘comeback’ nzuri ya Alikiba.
Bongo5 imewatafuta Alikiba na Tundaman ili kutaka kuthibitisha lakini kwa bahati mbaya simu zao wote hazikupokelewa.
Powered by Blogger.