"Muda wa kuvaa nusu uchi kwa wasanii umepitwa na wakati" Asema Batuli

Mwigizaji  mwenye mvuto Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amewataka wasanii wenzake wabadilike na kuvaa kama yeye kwani muda wa kuvaa nusu uchi  umepitwa na wakati.

Akizungumza nasi  baada ya kutupia picha yake aliyovaa gauni refu mtandaoni, Batuli alisema: “Muda wa kuvaa utupu umepita, wasanii tunapaswa tubadilike kwani kila siku tumekuwa tukisemwa vibaya na jamii.”

Batuli aliongeza kuwa, kama kila msanii wa kike atavaa kiheshima, wataheshimiwa na kuwa mfano wa kuigwa.

Powered by Blogger.