Baada ya UKAWA kutoka nje ya bunge jana, haya ni ya leo ya Samwel Sitta
Jana April 16 2014 UKAWA wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba wakati bunge likiwa katikati waligoma kuendelea nalo na kuamua kutoka nje kwa kile wanachosema ni ubaguzi na matusi pamoja na mapungufu mengine ambayo hawawezi kuyavumilia.Baada ya hayo mwenyekiti wa bunge la katiba Mh. Samwel Sitta leo April 17 2014 akatumia sekunde kadhaa tu baada ya bunge kuanza kwa kusema ‘hadi sasa hawajaniambia kama wametoka moja kwa moja au vp, kwa vyovyote vile jambo lile halikustahili.. katika nchi yoyote kwa Mwananchi kuteuliwa kuwa miongoni mwa wale ambao wanaaminiwa na nchi kutunga katiba mpya ya nchi ni heshima ya kipekee kabisa
‘Ni dhamana ambayo inatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wowote kwa sababu utungaji wa katiba ni jambo la mara moja pengine kwa vizazi viwili vitatu au miaka 50 kama kwetu hapa, baadhi yetu pengine hatujatambua uzito wa dhamana hiyo’