Tahadhari picha zinatisha..Watu wachinjana kiteto
Mapigano bado yanaendelea kati ya wafugaji wakimasai na wakulima eneo la Matui, chanzo kugombea maeneo ya kilimo na ufugaji, naomba serikali ichukue hatua maana hali ni mbaya sana, hamna hata polisi mmoja aliyeenda kutuliza gasia hizo, watu wengi wameshaanza kuyahama makazi yao kunusuru maisha yao, na inasemekana kuna kundi kubwa la wamasai kutoka Mererani na Simanjiro wamejipanga kwenda kuwasaidia wenzao.
Raia wafunga majumba yao na wamekusanyika katika kituo kidogo cha polisi Matui kwa ajili ya usalama wao.