Welbeck aiokoa Arsenal dakika ya 90 kwa sare dhidi ya Hull City

Bao la dakika ya 90 kupitia kwa mshambuliaji Danny Welbeck limeisaidia Arsenal kuepuka kipigo kutoka kwa Hull City kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu uliopigwa Emirates.

Hii inakuwa ni sare ya tano kwa Arsenal katika michezo minane waliyocheza, wakishinda mara mbili na kupoteza mara moja.
Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake mpya Alexis  Sanchez kunako dakika ya 13.

Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika tano tu kabla Mohamed Diame hajaizawazishia Hull City dakika ya 18 Abel Hernandez akapiga la pili dakika ya 46.






Wakati ngoma ikielekea kwisha kwa matokeo ya 2-1, Danny Welbeck akaisawazishia Arsenal.

Arsenal: Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Flamini (Ramsey 63), Wilshere (Campbell 69), The Ox, Cazorla, Alexis, Welbeck

Hull City: Harper (Jakupovic 43), Chester, Davies, Dawson (Bruce 84), Elmohamady, Huddlestone, Livermore, Robertson, Ben Arfa, Hernandez (Ramirez 63).
Powered by Blogger.