Kibaka apokea kichapo kikali Morogoro baada ya kupora simu
Wakihojiwa na Paparaziwetu eneo la tukio mashuhuda wa tukio hilo walisema "dada alikuwa akieleka SUA huku akiongea na simu ghafla boda boda huyu aliyekuwa amembeba mwenzake nyuma walimpitia na kumpora simu dada huyo na kukimbia nayo ambapo dada alipiga kelele za mwizi na boda boda wa kijiwe cha FK waliwasha pikipiki zao na kuwafukuza ambapo walifanikiwa kumkamata eneo la mazimbu reli ya pili ambapo mwenzake aliyempakia nyuma alifanikiwa kuruka katika pikipiki na kukimbia na kumuachia msala wote mwenzake.
Katika hatua nyingine mmoja wa boda boda aliyefanikisha kukamatwa kwa kibaka huyo alisema' Hii kazi ya boda boda ni kazi kama kazi nyingine na tunashukuru serikali inatutambua lakini kuna baadhi ya bodaboda wanatupaka matope kwa kufanya mambo ya wizi huku wakitumia mgongo wa boda boda ndio maana tulivyoshuhudia tukio hili tumeamua kuteketeza mafuta yetu na kuwafukuza vibaka hawa na kufanikiwa kuwakamata"alisema Bw Juma ldd
Mwandishi wa mtandao huu alipiga simu polisi kwa lengo la kumuokoa mwizi huyu ambapo fasta Defenda lilifika na kumchukua kibaka huyu ambapo baadhi ya watu wanaomfahamu walidai anaegesha pikipiki yake kijiwe cha Tumbaku lringa Road na kwamba pikipiki hiyo alikabidhiwa kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo alikuwa amebakiza miezi miwili kukamilisha mkataba huo.
Afisa mmoja wa jeshi la polisi aliyeomba hifadhi ya jina lake alimtonya mwandishi wetu kwamba boda boda huyo alikata roho siku iliyofuata.

Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Omar mkazi wa Mafisa Morogoro,ambaye ni dereva wa boda boda mwishoni mwa wiki iliyopita alipokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira akidaiwa kumpora simu mwanamke mmoja nayedaiwa kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine’ SUA’