Rais Magufuli Amteua Profesa Lema Kuwa Mwenyekiti wa TAA
Rais John Magufuli, amemteua Profesa Ninatubu Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Profesa Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia Agosti 20, 2015.
Taarifa iliyotolewa leo (Jumamosi) na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tangu Oktoba 20, 2016.

Profesa Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).