Mtuhumiwa mbaroni kwa kumbaka mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka 5



Mtoto wa miaka (5) mkazi wa Kijiji cha Kabuhima Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita amefanyiwa ukatili wa kinyama baada ya kubakwa na jirani yao.

Mtuhumiwa anayedaiwa kufanya kitendo hicho cha kikatili inadaiwa kuwa alimkuta mtoto huyo anacheza mlangoni kwao akiwa hajavalishwa nguo ya ndani na wazazi wake jambo lililpelekea kufanya ukatili huo.

Akizungumuza na mwandishi wa habari hizi mzazi wa mtoto huyo, Benjamini Juma akiwa kituo cha afya cha Uyovu akisubiri vipimo na matibabu ya mtoto wake (jina tunalo) alimtaja mtu anayedaiwa kufanya kitendo hicho kuwa ni Juma Manjariwa anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 28 ambaye wanaishi nyumba moja ya kupanga

Alisema mwanae alikutwa na mkasa huo wakati yeye akiwa ndani amepumzika baada ya chakula cha mchana saa 7:37 mchana ambapo mama wa mtoto alikuwa amekwenda kusuka kwa jirani.

Alisema aliamua kutoka nje na kukuta kijana huyo anatoka nje na kuanza kukimbia, huku mtoto akitokwa na damu nyingi sehemu zake za siri.

Mganga Mkuu wa kituo cha afya Kata ya Uyovu, Joshua Mazingo alisema, “Mimi nikiwa safarini nilipokea taarifa za mtoto huyo ambaye alifikishwa kwenye kituo cha afya kupimwa kisha kukutwa na mbegu za kiume na kwamba tunaendelea kumpima vipimo vingine kubaini kama ameambukizwa magonjwa mengine ya zinaa.”

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kubakwa kwa mtoto na kwamba polisi tayari wamemkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.


Powered by Blogger.