UZALENDO KWANZA: PIGA KURA UBORESHE MAISHA YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI
Shirika linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama "Tulip" itolewayo nchini Uholanzi. Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali.
Kwa kupiga kura hiyo bofya hapa