Steve Nyerere Atoa wosia kwa Bongo Muvi
MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa ana mengi ya kujivunia katika klabu hiyo ambayo anaamini yatawafanya wasanii wakumbuke kipindi cha uongozi wakeMsanii wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ Akipiga stori na paparazi wetu, Steve alisema kuna vitu vingi ambavyo ameifanyia Klabu ya Bongo Movie ikiwemo kurudisha heshima katika jamii kwa ujumla kuwa klabu hiyo haihusiani na vitendo vya kifuska bali ni wasanii wanaojiheshimu na kuthamini kazi zao kwa kukemea maovu.
“Naamini wasanii wa Bongo Movie watanikumbuka kwa mengi niliyowafanyia, hata kama wanatazama mabaya yangu lakini yapo na mazuri ambayo ni wazi hayapingiki, niliondoa matabaka pamoja na kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ni wazi jinsi ilivyo sasa ni tofauti na nilivyoingia madarakani, nimewakutanisha na fursa mbalimbali na kusimamia nidhamu,” alisema Steve.