Mwalimu agongwa na gari na kufariki papo hapo
Mwalimu mmoja mkazi wa Mlole Manisapaa ya Kigoma Ujiji amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace yenye namba CMS 688 inayofanya safari zake Kigoma mjini kwenda Kijiji cha Simbo wilayani humo.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa, Kamishna Msaidizi (ACP), Michael Deleli, alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 2:00 asubuhi na kumtaja aliyefariki kuwa ni Godness Masuruli (30), aliyekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari hilo lililokuwa likiendeshwa na John Makosa (34).
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake huku dereva akiwa mahabusu na atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake.
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake huku dereva akiwa mahabusu na atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake.