Madereva wa mabasi ya UDA wamegoma kuingia kazini leo
Madereva wa Kampuni ya Usafi jijini Dar es Salaam (UDA), leo wamegoma kuingiza mabasi barabarani kwa kinachoelezwa ni madai mbalimbali ya haki zao dhidi ya shirika hilo.
Kwa mujibu wa dereva mmoja ambaye hakupenda kuweka wazi jina lake, wamefikia hatua hiyo kufuatia uongozi wao kutosikia kilio chao cha kupunguziwa kiasi cha fedha wanachotakiwa kukipeleka kwa siku.
Kwa mujibu wa dereva mmoja ambaye hakupenda kuweka wazi jina lake, wamefikia hatua hiyo kufuatia uongozi wao kutosikia kilio chao cha kupunguziwa kiasi cha fedha wanachotakiwa kukipeleka kwa siku.
Dereva huyo alisema kuwa, hesabu wanayotakiwa kupeleka ni shilingi 205000 kwa njia zote ambayo ni nyingi sana.
Aliongeza licha ya kuuomba uongozi upunguze kiasi hicho hadi kufikia shilingi 160,000 wamegoma, pia wamekuwa wakicheleweshewa mishahara ambapo mshahara wa mwezi uliopita hawajalipwa hadi leo, kutowekewa fedha za NSSF.
Dereva huyo aliongeza kuwa kero nyingine ni pale inapotokea wamekamatwa kwa makosa ya barabarani na kuwekwa mahabusu, wao huyafuata magari yao tu na kuwaacha wao wakisota ndani.
Madereva hao wanaomba kukutana na uongozi wa juu wa shirika hilo ili kukaa na kuzungumza nao kwa lengo la kufikia muafaka.
Mgomo huo umeleta usumbufu kwa wakazi wengi wa jiji hususani wa Mbagala ambapo wafanyakazi wengi leo wamechelewa kufika maofisini na kwenye shughuli zao zinazowapatia kipato.
crdt GPL