Lori lililobeba Ng'ombe lapata ajali Ubungo-Dar

Mfanyabiashara mmoja wa mifugo (ng’ombe) na dereva waliokuwa katika lori lililokuwa limebeba mifugo hiyo, leo wamenusurika katika ajali iliyotokea asubuhi eneo la Ubungo-Mataa, jijini Dar es Salaam.

Gari hilo lililokuwa limebeba ng’ombe wapatao thelathini likitokea Wilayani Kondoa, Dodoma, limepata ajali na ng’ombe kadhaa kuumia sehemu mbalimbali za miili.
  Wakizungumza na mtandao huu, mashuhuda wamesema tukio hilo lilifuatia mwendesha pikipiki (bodaboda) kukatiza kwa kasi mbele ya gari hilo na dereva alipoamua kuwakwepa, gari lilianguka.

Aidha mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma, amelipongeza jeshi la polisi na askari kwa ulinzi walioufanya hapo kwani hakuna kitu kilichopotea.
Powered by Blogger.