Facebook Kutumika Kutoa mafunzo ya Usalama barabarani
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha mafunzo katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua uwanja zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ajali.
Aidha amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na kuondoa tuhuma za rushwa.

Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph, akisalimiana na Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, mara baada ya kuwasili kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.