Majambazi watano wakamatwa na risasi 112, meno ya tembo na bunduki.
Operesheni maalum iliyoshirikisha askari polisi wa mikoa ya Morogoro na Dodoma, imefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa watano wanaodaiwa kuhusika na matukio ya ujambazi na ujangili, sambamba na bunduki moja aina ya smg, magazine tatu, risasi 112 na meno mawili ya tembo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumetokana na polisi Dodoma kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja wa ujambazi aliyewezesha kupatikana kwa wenzake watatu mkoani Morogoro, akiwemo mwanamke mmoja, ambao majina yao yamehifadhiwa kwasababu za kiupelelezi, pamoja na mtuhumiwa mwingine wa ujangili, aliyekamatwa na vipande viwili vya meno ya tembo, huko kata no 14, tarafa ya mikumi katika wilaya maalum ya kipolisi ya Ruhembe.
Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepongeza jitihada zilizofanywa na askari polisi wa Morogoro kwa kushirikiana na polisi wa Dodoma, na kutoa wito ushirikiano huo uendelee hata katika mikoa na wilaya nyingine zinazopakana na Morogoro, na wananchi waendelee kutoa ushirikiano wa kuwafichua wahalifu, ili kukomesha kabisa vitendo vya kiuhalifu vinavyoendelea.
Source ITV