Jeshi la polisi lakamata bunduki 7 na mabomu Mkoani Geita

Habari zilizotufikia hivi punde ambazo bado siyo rasmi zinasema kuwa jeshi la polisi mkoani  Geita limekamata bunduki saba na mabomu 10 eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe.

Inasadikiwa kuwa bunduki hizo ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  usiku wa kuamkia jana na kujeruhi askari wawili.
Bunduki 7 na mabomu 10  yaliyokamatwa huko Bukombe

Tunaarifiwa kuwa Bunduki zilizokamatwa nne ni SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuru la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinasema kuwa  katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi linaloendelea kufanya kazi nzuri  limekamata watu watatu  pia  na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Ushirombo anayedaiwa kushiriki katika tukio la jana.

Tumearifiwa kuwa  jeshi la polisi linaendelea kufanya msako mkali ili kuwakamata wahusika wote na silaha zote zilizoporwa na majambazi.

Tunasubiri jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo
Powered by Blogger.