Inasikitisha.. Baba amnyonga mwanaye na kumzika
Mtoto wa umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey aliyeuawa kikatili kwa kunyongwa kisha kuzikwa na baba yake mzazi, Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’ (27) kwa kuwa alizaliwa akiwa ametanguliza makalio yake, amezidi kuibua maswali.
Baadhi ya wakazi wa Katavi waliozungumza na gazeti hili juzi, walihoji uhalali wa baba kumjadili mtoto katika kuzaliwa kwa sababu ya kutanguliza kiungo fulani.Wengine walitaka kujua ni kwa nini kama kumuua mtoto wake, mzazi huyo alisubiri kwa mwaka mmoja na miezi miwili? Mtuhumiwa ambaye pia ni mganga wa kienyeji anayeishi Kitongoji cha Mwikang’ombe, Kijiji cha Katuma wilayani Mpanda, alitenda unyama huo kwa madai kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa ametanguliza makalio, hivyo ni nuksi kubwa katika shughuli zake za uganga wa kienyeji, madai yaliyopingwa na watu mbalimbali, zikiwemo taasisi za kutetea haki za binadamu.

Mtuhumiwa Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’( katikati) aliyemuua mwanaye mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, alidai mzazi huyo alitenda uhalifu huo Agosti 20, mwaka huu ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi, Agosti 26.
Ilidaiwa siku hiyo ya tukio, mtuhumiwa huyo baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake, alimzika kwa siri katika kibanda chake anachofanyia shughuli za uganga.
Kamanda Kidavashari alisema mtoto Regina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari.
“Ndipo baba mzazi wa binti huyo alipomchukua marehemu na kwenda kumuuguza kwa siri pasipo mama yake mzazi kufahamu kwani alimdanganya kuwa mtoto wao amepelekwa kutibiwa na babu yake mkoani Mwanza,” alisema Kidavashari.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakazi wa kitongoji hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao, walimtilia shaka mtuhumiwa kutokana na tetesi zilizosambaa kwamba, Regina aliuawa na baba yake mzazi na kuzikwa kwa siri.
Mwenyekiti huyo na wakazi wa eneo hilo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa na kuhoji alipo binti yake, aliposhindwa kujibu wakasema wampekue ambapo alipinga vikali lakini alipopekuliwa kibandani kwake walibaini kuwepo kwa tuta dogo lililokuwa limechimbwa siku za karibuni.
Wakazi hao walifukua tuta hilo na kukuta kichwa cha mtoto Regina na ndipo wakalitaarifu jeshi la polisi.
Mama wa marehemu, Maria Exavery (22) alisema hakupewa taarifa kwamba binti yake amekufa.
“Mimi nilikuwa nafahamu Regina yuko kwa babu yake Mwanza akitibiwa,” alisema huku akimwaga machozi.
Naye Regina Kaboni (40), mkazi wa Isamilo Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na mtuhumiwa, anadai kuwa alishirikishwa katika maziko ya binti huyo baada ya kufa.“Hata hivyo, nilishtushwa sana kwa kitendo cha mtuhumiwa kumzika mwanaye bila mkewe, nilipomuuliza akadai mila za kwao mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio, mama mzazi wa mtoto ni mwiko kushirikishwa katika maziko.
Kwa mujibu wa Kidavashari watu wanne, wakiwemo wazazi wa marehemu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ambapo watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika.
Wengine wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Regina Kaboni na Msolwa Jacob (29), mkazi wa Kitongoji cha Mwikang’ombe.