Watu zaidi ya 17 wapoteza maisha katika ajali ya basi mkoani Tabora
Watu zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka kijiji cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea jana jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.

Hali ni tete sana eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Katavi kugongana uso kwa uso. Dreva wote wa mabasi hayo wamefariki hapo hapo, mmoja akiwa amekatika kichwa.
Abiria kadhaa wakiwa wamenasa katika mabasi hayo, baadhi wakiwa wamekatika mikono na miguu. Abiria wapatao watano wamefariki hapo, na majeruhi zaidi ya 30 wamepelekwa katika Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.